Kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), imekutana mkoani Iringa ili kupata uwelewa wa pamoja na kuweka mikakati ya utekelezaji na ufanikishaji wa maadhimisho hayo.
Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya wiki ya REGROW, Hobokela Mwamjengwa ameeleza kuwa lengo la wiki hiyo ni kuhabarisha wadau wa mradi na Watanzania kwa ujumla kuhusu mradi, fursa zilizoibuliwa, maeneo ya uwekezaji na wanufaika wa mradi kwa maslahi Taifa.