Maandalizi Utoaji Tiba Ya Kupandikiza Uloto (Bone marrow) Wakamilika Muhimbli.

0
247

Wagonjwa wa Saratani ya Damu, Seli Mundu na magonjwa mengine ya damu wataanza kunufaika na tiba ya magonjwa hayo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukamilika kwa maandalizi ya utoaji tiba ya kupandikiza Uloto (Bone marrow) hapa nchini.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbli Dokta Hedwiga Swai amesema serikali imetoa Shilingi Bilioni sita Nukta Mbili kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na miundombinu ya utoaji wa tiba hiyo.

Akifafanua kuhusu tiba ya upandikizaji Uloto kwa wagonjwa mkuu wa kitengo cha Magonjwa ya Damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dokta Stella Rwezaura amesema chembechembe mama huvunwa kutoka katika Uloto unaopatikana ndani ya mfupa wa mchangiaji na kupandikizwa kwa mgonjwa.

Kuanza kutolewa huduma hiyo hapa nchini mwishoni mwa mwaka huu kutaokoa fedha na kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa ya damu ambapo kwa mujibu wa takwinu za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wagonjwa 130 hadi 140 huhitaji tiba ya kupandikiziwa Uloto kwa mwaka.