Maambukizi ya VVU yaongezeka GEITA

0
282

Maambukizi ya Virusi vinavyoambukiza Ukimwi mkoani Geita yameongeza kwa asilimia 0.3 kutoka asilimia 4.7 mwaka 2011/2012 hadi asilimia Tano mwaka 2016/2017 na hivyo kutishia kupungua kwa nguvu kazi ya Taifa.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa wilaya ya Geita,- Josephat Maganga wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambapo kwa mkoa wa Geita yamefanyika katika viwanja vya CCM Kalangalala.

Maganga amesema kuwa, maambukizi mapya ya Virusi vinavyosababisha Ukimwi mkoani Geita yapo zaidi kwa Vijana na Wanawake.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwa mwaka huu ni “Jamii ni Chachu ya Mabadiliko, Tuungane Kupunguza Maambukizi ya VVU.