Maagizo matano kwa Wizara ya Madini

0
133

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa maagizo matano kwa Wizara ya Madini na sekta zinazohusika ili kuhakikisha zinaboresha sekta ya madini nchini.

Maagizo hayo ni;

  1. Kusimamia utekelezaji wa maadhimio yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Kimaataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania mwaka 2022,  ili taarifa za utekelezaji ziwasilishwe kwenye mkutano ujao.
  2. Wizara ya Madini kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vidhibiti utoroshaji wa madini, na kuhakikisha biashara hiyo inafanyika kisheria.
  3. Wizara iimerishe ushirikishwaji wa wadau kwenye masuala mbalimbali kwa kuimarisha mawasiliano na wadau wa madini, ili kuwa na mfumo sahihi wa kuwasilisha na kutatua changamoto zinaazowakabili.
  4. Wizara kwa kushirikiana na TAMISEMI zibainishe na kutambua maeneo ya  masoko na viwanda vya madini.
  5. Wizara hiyo iendelee kuvinadi viwanda vya ndani kwa kazi vinavyofanya ikiwemo  kusafisha madini, ili kuvutia wateja kutoka ndani na nje ya nchi.