Maafisa Wanafunzi 128 wa JWTZ watunukiwa Kamisheni

0
214

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Magufuli ametunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 128 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Hafla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa hao wapya  kwa cheo cha Luteni Ussu imefanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Maafisa hao wametunukiwa Kamisheni baada ya kuhitimu mafunzo yao katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kilichopo mkoani Arusha, mafunzo yaliyoanza tarehe 28 mwezi Januari mwaka 2019.

Mafunzo hayo yalipoanza walikua Maafisa 126 lakini 26 wameshindwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali.

Maafisa 28 ambao nao wametunukiwa Kamisheni na kufanya idadi hiyo ya 128 wamehitimu katika vyuo vya Kijeshi vilivyopo kwenye nchi za China, Uingereza, India, Ujerumani, Kenya na Morocco.

Wakati wa hafla hiyo Maafisa waliofanya vizuri wakati wa mafunzo hayo wamepewa zawadi.