Maafisa wa TRA washikiliwa kwa tuhuma za rushwa

0
268

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU) mkoani Manyara inawashikilia maafisa watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  mkoani humo, kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja kutoka kwa mfanyabiashara wilayani Babati.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkuu wa TAKUKURU wa mkoa wa Manyara, –  Holle Makungu amewataja watumishi hao kuwa ni Eva Mtandika, Jackline Manjira na Ephraim Medard ambao wote ni watumishi wa TRA mkoa wa Manyara.

Makungu ameongeza kuwa uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa mfanyabiashara huyo alikadiriwa kulipa kodi ya shilingi laki mbili na nusu kwa mwaka, lakini maafisa hao walimueleza kuwa amefanyiwa makadirio madogo na hivyo kumtaka alipe shilingi milioni moja ili asifikishwe mahakamani.