Serikali imewataka Maafisa Uhamiaji katika mikoa ya pembezoni mwa nchi kuacha kuwanyanyasa wananchi kwa kutumia muonekano wao wa maumbile na kuwalazimisha kuimba wimbo wa Taifa kama vigezo katika kubaini uraia wao.
Akizungumza na wananchi wilayani Ngara mkoani Kagera, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amewataka maafisa uhamiaji hao kutumia utaalam wao kuondoa kero na malalamiko dhidi yao.
Waziri Lugola ametoa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya wilaya ya Ngara kuhakikisha inanunua vifaa vya kujikinga na moto katika taasisi zilizo chini yake ikiwemo shule na vituo vya afya.