Maadhimisho ya wiki ya maji kwa mwaka huu yafutwa

0
123

Wizara ya Maji imefuta shughuli zote zilizokua zifanyike kuelekea siku ya Maji Duniani, ikiwa ni kuchukua tahadhari dhidi ya maambulizi ya virusi vya corona.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na wizara hiyo imeeleza kuwa, hafla za uzinduzi wa miradi ya maji na mikutano yote ambayo ilikua ifanyike katika wiki ya maji imefutwa.

Maadhimisho ya wiki ya Maji Kitaifa yalipangwa kuzinduliwa hapo kesho na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan huko Mbweni mkoani Dar es salaam.

Kufuatia kuthibitika kuwepo kwa mgonjwa wa homa ya corona nchini, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewatahadhrisha Watanzania wote kuepuka msongamano, ili kujiepusha na maambukizi ya virusi hivyo.