Lukuvi ateta na wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi

0
238

Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi amewataka wadaiwa wote wa kodi ya pango la ardhi kulipa kodi na malimbikizo ya madeni yao kabla ya tarehe 20 Juni mwaka huu.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo Jijini Dodoma katika kikao chake na Wakuu wa Taasis,Mashirika na Makampuni yanayodaiwa kodi ambapo amesema atakae kaidi agizo hilo serikali itabatilisha umiliki wake wa ardhi na kunadi ardhi yake pamoja na kufunga ofisi zao zote.

Waziri Lukuvi pia amesema Taasis ambazo hazitalipa kodi ya Pango la ardhi ni zile ambapo ardhi yao hazifanyiwi biashara na kuzitaka Taasis hizo kuandika barua ya kuomba msamaha wa kodi ya Pango la ardhi.

Amesema Wadaiwa wote wanatakiwa kuhakiki madeni yao na kulipa kwa mifumo mbali mbali ya kimtandao ikiwemo njia za simu jambo ambalo baadhi ya wadaiwa wameahidi kutekeleza agizo hilo.

Jumla ya Taasis,Mashirika na Makampuni 207 zinadaiwa kodi ya Pango la ardhi deni ambalo ni sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 200.