Lugha Ya Kiswahili Yaanza Kutumika Rasmi SADC

0
224

WAKUU wa Nchi na Viongozi wa Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)wamepitisha kwa kauli moja lugha ya kuwa lugha rasmi ya nne itakayotumika kwenye jumuiya hiyo.
Kupitishwa kwa lugha hiyo kumetokana na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais Dk.John Magufuli kuomba lugha hiyo iingizwe kwenye jumuiya hiyo.


Akizungumza leo Agosti 18,2019 kwenye ufungaji wa Mkutano Mkuu wa 39 wa SADC ambao umefanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere Mwenyekiti huyo mpya ametoa taarifa ya kupitishwa kwa lugha ya Kiswahili kuwa rasmi.


“Nianze kutoa hotuba yangu ya kufunga mkutano wa 39 wa SADC kwa kueleza hapa,nilitoa ombi kuhusu lugha ya Kiswahili kutumika kwenye SADC.Wakuu wanachama wameiteualugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya  nne ya SADC.
“Narudia tena nawashukuru wakuu wa nchi na wakuu wa Serikali kwa kukubali lugha hiyo iwe rasmi kwenye jumuiya yetu.Baba wa Taifa amekuwa na heshima kubwa sana katika Bara la Afrika.

Katika maisha wapo wanajitolea kwa mambo mbalimbali, wapo wanatoa figo,wapo wanaotoa fedha na utoaji wa aina nyingine,” amesema.


Amefafanua Mwalim Julius Nyerere yeye aliamua kutoa upendo na maisha yake kwa ajili ya wengine na hivyo sehemu kubwa ya maisha aliyatumia kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa salama  na ndio maana nchini Tanzania kuna maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa kambi za wapigania uhuru na hasa nchi za Kusini mwa Afrika.


” Mwalimu Nyerere alishiriki kwa vitendo kwa ajili ya kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa huru.Tanzania imekuwa na kambi nyingi za wapigania uhuru na mojawapo ilikuwa eneo la Kongwa ambako anatoka  Spika wa Bunge Job Ndugai.