Lori lagonga magari matano

0
179

Lori aina scania lililokuwa likifanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Jamhuri ya KIdemokrasi ya Congo (DRC) limeyagonga magari matano katika eneo la Iwambi mkoani Mbeya, na kusababisha moto mkubwa uliounguza magari mawili likiwemo lori hilo.

Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa ni lori hilo ambalo lilibeba shehena ya kopa kufeli breki.

Habari zaidi kutoka mkoani Mbeya zinaeleza kuwa, gari la zimamoto lilifika katika eneo la tukio na kushindwa kuuzima moto huo, na kulazimu gari la zimamoto kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe kwenda kufanya kazi hiyo.