Longido wapata neema ya maji

0
161

Rais Samia Suluhu Hassan leo katika ziara yake mkoani Arusha amezindua kiwanda cha Nyama cha Eliya Food Overseas kilichopo Longido mkoani humo.

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan amezindua mradi mkubwa wa maji Longido utakaowanufaisha wananchi zaidi ya 13,000.

Mradi huo wa maji Longido umegharimu bilioni 4.5 na utapeleka maji katika Mji wa Namanga na kuwaondolea kero ya maji wananchi wa mji huo.