Liundi: Uteuzi uwaangalie wahitimu NDC

0
134

Mwenyekiti wa wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Fred Liundi, amewasilisha maombi matatu kwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akisoma salamu za wahitimu wa chuo hicho katika sherehe za maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwake.

Maombi aliyowasilisha ni pamoja na kumuomba Rais kutenga muda kila mwaka kutembelea chuo hicho na kutoa mhadhara ili kuwajengea uzalendo wanafunzi, pia amemuomba awaruhusu Mawaziri wa Wizara mbalimbali kufika chuoni hapo kwa ajili ya kubadilishana uzoefu hali itakayosaidia uwajibikaji wenye uweledi.

Ombi la tatu alilowasilisha Mwenyekiti huyo ni kumuomba Rais kuangalia wanafunzi wanaotoka chuoni hapo pindi anapofanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, kwani wahitimu wanaotoka hapo wamefundishwa namna bora ya kufanya maamuzi katika uongozi.