Lishe duni chanzo cha magonjwa na udumavu

0
355

Baadhi ya watafiti wa afya wamebaini uwepo wa magonjwa yanayochangiwa na lishe duni na hivyo kusababisha udumavu wa makuzi kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Bodi ya Asasi inayojishughulisha na maendeleo ya kilimo cha mazao lishe (TAHA), Edith Banzi wakati wa uzinduzi wa siku ya afya na lishe katika Kata ya Marangu Magharibi wilayani Moshi.

Edith amesema jamii nyingi zimeacha kutumia vyakula vya asili ambavyo vina viini lishe badala yake wamekuwa wakila vyakula visivyo na viini lishe.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kyala wamesema hawana uelewa wa masuala ya lishe na matunda kutokana na kutofikiwa na elimu stahiki jambo linalochangia kuongezeka kwa wakazi wenye udumavu wa afya.

Akizindua siku ya afya na lishe, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaji Kundya amewataka wazazi kuwasimamia watoto katika kuhakikisha wanapata chakula bora kwa ajili ya makuzi yao kiafya na kiakili.

Kaulimbiu ya siku ya afya na lishe mwaka huu ni Chakula Bora, Kinga yako, Dawa yako.