Lijuakali kuchukuliwa hatua na Bunge

0
450

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kumchukulia hatua Mbunge wa jimbo la Kilombero mkoani Morogoro, -Peter Lijualikali, kufuatia tuhuma za kutoa kauli za kejeli na dharau dhidi ya Spika na Ofisi ya Bunge.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Ofisi ya Bunge imesema kuwa Mbunge Lijuakali alitoa kauli hizo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Spika wa Bunge, – Job Ndugai anatafakari hatua za kinidhamu za kumchukulia Lijualikali.