Libya Waikomboa Kambi ya Naqliya

0
272

Jeshi la Serikali nchini Libya limefanikiwa kuikomboa kambi ya Naqliya iliyopo jirani na mji wa Tripol  iliyokuwa ikishikiliwa na wapiganaji wanaomtii Jenerali Halifa Haftar anayeendeleza harakati za kuuteka mji wa Tripol.

Taarifa kutoka nchini humo zinaarifu kuwa, vikosi hivyo vya jeshi la serikali inayotambuliwa na umoja wa mataifa, vilifanya oparesheni maalumu iliyofanikisha kuikomboa kambi hiyo ambapo katika oparesheni hiyo wapiganaji kumi na wanane wa Jenerali Haftar wameripotiwa kuuawa.