Leyla Sheikh kuzikwa Tanga

0
174

Mazishi ya Leyla Sheikh, mmoja wa Waasisi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa chama hicho yatafanyika kesho Juni 13, 2023 mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAMWA, Leyla Sheikh aliyezaliwa Januari 08, 1958 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo June 12, 2023.

Leyla Sheikh atakumbukwa kwa kuwa Mwandishi wa Habari mahiri na mtetezi wa haki za Wanawake na Wasichana.