Lema aachiwa kwa dhamana

0
369

Jeshi la polisi mkoa wa Singida limemwachia kwa dhamana Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema baada ya kumshikilia kwa muda wa siku tatu katika kituo kikuu cha polisi cha mjini Singida.

Lema alikua akishikiliwa kwa ajili ya mahojiano baada ya kutuhumiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya watu 14 wilayani Manyoni mkoani humo, ambapo alisema kuwa watu hao waliuawa kwa kuchinjwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini anadaiwa kutoa taarifa hizo kwenye mazishi ya Katibu wa Chama Cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Manyoni Mashariki, ambaye aliuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kukatwa na vitu vyema ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.

Wakili anayemtetea Lema, -Hemed Kulungu amesema kuwa Mbunge huyo anatakiwa kuripoti polisi Singida machi 24 mwaka huu.