Le Mutuz kuzikwa Jumatano Dodoma

0
132

Mwili wa William Malecela maarufu Le Mutuz, utazikwa Jumatano mkoani Dodoma.

Leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ndugu, jamaa na marafiki wameuaga mwili wa Le Mutuz wakiongozwa na baba yake, Mzee John Malecela.

Baada ya mwili huo kuagwa, umesafirishwa na ndege ya Serikali kwenda Dodoma kwa ajili ya mazishi.

Le Mutuz alikuwa Mmiliki na Mkurugenzi wa Le Mutuz Online TV na mmiliki wa Le Mutuz Blog.

Alifariki dunia Mei 14 mwaka huu mkoani Dar es Salaam.