Halmashauri ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imesema kuwa itaendelea kudhibiti utoroshaji wa kokoa katika halmashauri hiyo ili kuongeza mapato.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Dkt Hunter Mwakifuna mara baada kumalizika kwa kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo kilichokua kikijadili mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 .
Dkt Mwakifuna amesema kuwa tangu utoroshwaji huo wa kokoa kwenda nje ya wilaya hiyo Kyela kuanza kudhibitiwa mwaka 2017, mapato ya halmashauri hiyo yameongezeka kwa asilimia 90 hadi kufikia hivi sasa.
Kufuatia utoroshaji huo wa kokoa wilayani Kyela, Dkt Mwakifuna ametoa wito kwa wakulima wa zao hilo wilayani humo kuuza kokoa yao katika vyama vya ushirika, hatua ambayo pamoja na mambo mengine itasaidia kuongeza mapato ya halmashauri ya wilaya hiyo.
