Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani amesema kuwa, kwa sasa yeye si Mwanachama wa chama chochote.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Sumaye amesema kuwa ameamua kukaa pembeni ili aweze kutumika na chama chochote kile cha siasa kitakachohitaji msaada kutoka kwake.
Ameongeza kuwa, imezoeleka Mwanachama yeyote anapofikia uamuzi kama wake kuna baadhi ya watu wanasema kanunuliwa na chama kingine, lakini kwake yeye jambo hilo halipo.
Sumaye amefafanua kuwa, sababu kubwa ya kuondoka CHADEMA na kuachana na siasa ni kuona ushauri wake aliokua akiutoa kwa lengo la kukiendeleza chama hicho umekua ukipuuzwa na uongozi wa juu wa chama hicho.