Kwa mara ya kwanza Rais Magufuli ashiriki Misa Chamwino

0
217

Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli, leo wameshiriki Misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maria Imaculata,- Chamwino mkoani Dodoma.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli na familia yake kushiriki katika Misa ya Jumapili kwenye Parokia hiyo toka
ahamie rasmi mkoani Dodoma.

Wakati wa Misa hiyo, Rais Magufuli alipewa nafasi ya kuongea na Waumini mbalimbali wa Parokia hiyo ya Mtakatifu Maria Imaculata, ambapo amewashukuru kwa kumpokea na kuwaahidi kushirikiana nao.