Daktari bingwa wa magonjwa ya familia Davis Rubagumya amesema, kupata mtoto Njiti sio sababu ya kukata tamaa na kwamba jambo muhimu ni kuhakikisha mtoto huyo anapata malezi stahiki.
Dkt. Rubagumya
ameyasema hayo katika kupindi cha Jambo Tanzania cha TBC 1, ikiwa leo ni maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani.
Ameziasa familia kuacha kuhusisha suala la mtoto Njiti na mambo ya imani na kwamba juhudi za kibindamu pia zinahitajika kunusuru maisha ya mtoto.