Kunenge kutatua kero za Wazee Dar es salaam

0
178

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, -Aboubakar Kunenge amekutana na kufanya mazungumzo na Wawakilishi wa Wazee wa mkoa huo kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili ili Serikali iweze kuzifanyia kazi.

Katika kikao hicho, Kunenge amepokea changamoto na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Wazee hao, ambapo zipo changamoto zililizopatiwa majibu ya papo kwa papo na nyingine za kisera na kisheria ambazo ameahidi kuzifikisha katika ngazi husika.

Amewashukuru na kuwapongeza Wazee wote wa mkoa wa Dar es salaan kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya Katika kueneza busara, hekima na maarifa kwa jamii, jambo linalosaidia kuwa na kizazi kinachofuata maadili na kulinda amani na usalama mkoani humo.

Amewaeleza Wazee hao kuwa, ofisi yake iko wazi kupokea na kusikiliza ushauri kutoka kwao na kwamba ataweka utaratibu wa kukutana nao kila baada ya miezi mitatu.

Wazee wa mkoa wa Dar es salaam walioshiriki kikao hicho wamemshukuru Mkuu wa mkoa Kunenge kwa namna anavyowakumbuka na kuwathamini na wamemuahidi watampatia ushirikiano wa kimawazo Katika kila jambo.