Kundo : Tunaendelea na maboresho sekta ya habari

0
163

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew
amesema, Serikali inaendelea na kazi ya kuboresha mambo mbalimbali katika sekta ya habari nchini.

Mambo hayo ni pamoja na kukuza teknolojia ya kidijiti kwa lengo kuongeza mapato na kutoa fursa za ukuaji wa sekta ya habari nchini.

Mhandisi Kundo ametoa kauli hiyo jijini Zanzibar wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yanayoshirikisha waandisii wa habari kutoka vyombo mbalimbali ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi.

Tanzania, Leo inaungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha Siku hiyo ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu inayosema kuwa ‘Kuunda Mustakari wa Haki – Uhuru wa Kujieleza kama kichocheo cha Haki nyingine za Binadamu’.