Watanzania leo wanakumbuka miaka 50 tangu kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume kilichotokea Aprili 7 mwaka 1972.
Sheikh Abeid Amani Karume aliyeiongoza Zanzibar
baada ya Mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964, alizaliwa Agosti 4 mwaka 1905.
Aliuawa kwa kupigwa risasi ndani ya ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui, Unguja wakati akicheza bao na marafiki zake.