Kongamano la mapambano dhidi ya rushwa

0
120

Wakuu wa Taasisi mbalimbali na wadau wa Kuzuia na Kupambana na rushwa Barani Afrika wapo jijini Arusha kuadhimisha Siku ya Kupambana na Rushwa Afrika, inayofikia kilele chake Julai 11, 2023.

Leo linafanyika kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye sekta ya elimu na mitandao ya kijamii pamoja na wajibu wa jamii katika kupambana na rushwa.