KMC uso kwa uso na Azam FC

0
233

Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inaendelea  hii leo kwa mchezo mmoja kuchezwa  ambapo watoza ushuru wa Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es salaam  – KMC wanashuka dimbani kuwaalika Azam FC katika mchezo utakaochezwa kwenye dimba la uhuru.

Mchezo huo ambao ni wa kiporo unazikutanisha timu hizo ambazo zilikuwa zinaiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika iliyofanyika mwishoni mwa juma lililopita ambapo KMC wameondolewa katika michuano hiyo huku Azam FC wao wakifanikiwa kusonga mbele.

Hata hivyo mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa kocha wa Azam FC, -Etiene Ndariyagije dhidi ya waajiri wake wa zamani KMC huku kila timu ikipewa nafasi ya kuibuka na ushindi kutokana na ubora wa vikosi vyao.

Hapo kesho wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika – Yanga, wataanza msimu mpya wa Ligi Kuu kwa kumenyana na Ruvu Shooting Stars, huku bingwa mtetezi Simba akishuka dimbani siku ya Alhamisi kupepetana na JKT Tanzania.