Kivuko cha MV Kilindoni chazinduliwa

0
158

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua Kivuko cha MV Kilindoni kitakachokuwa kikitoa huduma za usafiri wa majini kati ya kisiwa cha Mafia na Nyamisati mkoani Pwani.
 
Akizindua kivuko hicho jijini Dar es salaam kilichojengwa na Kampuni ya Songoro Marines, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kupatikana kwa kivuko hicho ni utekezaji wa ahadi za Serikali za kutatua kero za wananchi ikiwemo usafiri wa majini.
 
Amesema pamoja na ujenzi wa kivuko hicho na vingine, bado ahadi ya kujenga meli kubwa itakayotoa huduma za usafiri katika bahari ya Hindi kati ya ukanda wa Pwani na Visiwa vya Comoro ipo palepale.
 
Kivuko cha MV Kilindoni kimegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni Tano, na kina uwezo wa kubeba abiria mia mbili, magari kumi na mizigo tani mia tano.