Kiungo cha msaliti

0
106

Malkia wa viungo (Iliki) ambacho ni kiungo chenye kufanya kazi nyingi ikiwemo kutengeneza dawa ama kuongeza ladha kwenye vinywaji na vyakula, wakati mwingine huitwa kiungo cha msaliti (Cheater’s spice).

Watumiaji wa kiungo hiki haswa Pwani ya Tanzania husema kuwa walevi na wavutaji sigara hutembea na punje kadhaa za iliki na kuzila mara baada ya kunywa au kuvuta ili kuondoa kabisa harufu ya pombe na sigara na huweza kudanganya kuwa hawakutumia vitu hivyo bila mtu kujua ukweli.