Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani chafunguliwa

0
261

Rais John Magufuli  na Rais Edgar Lungu wa Zambia, wamefungua Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande wa Nakonde Zambia na katika mji mdogo wa Tunduma nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Rais Magufuli ametangaza kumpatia
Rais Lungu Tani 25 za korosho bure na Tani 25 nyingine Rais huyo atazinunua kutoka Tanzania.

Korosho hizo zitasafirishwa kwenda nchini Zambia kabla ya Oktoba 12 mwaka huu.