Kitabu cha Mzee Mkapa chagharimu shilingi Milioni 230

0
237

Kitabu cha Maisha yangu, Kusudio langu kinachozinduliwa hii leo na Rais John Magufuli, kimeigharimu Taasisi ya Uongozi Shilingi Milioni 230 kwa ajili ya kukiandaa na kukichapisha.

Kitabu hicho chenye kurasa 315 zenye sura Tisa, kimeandika na yeye mwenyewe Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin Mkapa na kupigwa chapa na kampuni ya Kitanzania ya Mkuki na Nyota.

Akisoma muhtasari wa kitabu hicho jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja amesema kuwa, imewachukua muda wa miaka mitatu kuandaa, kuhakiki na kuchapisha kitabu hicho.

Kitabu hicho kinazinduliwa hii leo, siku ambayo pia ni ya kuzawaliwa kwa Mzee Mkapa ambaye anafikisha umri wa miaka 81.