Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Venance Mabeyo jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha mtoto wake Nelson, ambaye ni Rubani aliyefariki Dunia hii leo katika ajali ya ndege ndogo huko Serengeti mkoani Mara.
