Kiswanglish kiishe Bungeni : Dkt. Mpango

0
259

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuacha kutumia lugha ya kiswahili na kingereza kwa pamoja (Kiswanglish) wawapo bungeni.

Dkt. Mpango amesema hayo wakati akifungua Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani linalofanyika jijini Arusha, na kukutanisha vyombo vya habari duniani vinavyotangaza lugha ya Kiswahili.

Pia Dkt. Mpango amegusia suala la Watangazaji wa vyombo vya habari kutumia lugha isiyo rasmi kwenye utangazaji, hali inayosababisha Kiswahili kukosa thamani kwa watumiaji.