Kiswahili kiendelee kutumika Sekondari

0
166

Serikali imetoa taarifa kwa wananchi wote ndani na nje ya nchi kutambua kwamba, hakuna mabadiliko yaliyofanyika kuhusu ufundishaji wa somo la Kiswahili katika Shule za Sekondari kwani Kiswahili ndiyo lugha ya Taifa na hilo halina mabadiliko, na ni lugha iliyopewa hadhi ya kutumika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika pamoja na Umoja wa Afrika.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya  Rais-TAMISEMI imesema kumekuwepo na za upotoshaji kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye shule za Sekondari.

“Ofisi ya Rais -TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeona mijadala na taarifa mbalimbali zisizosahihi kuhusu ufundishaji wa somo la Kingereza na kufungia matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye shule za Sekondari.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeona vyema kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo kuwa Serikali katika mabadiliko ya mitaala ya mwaka 2010 na Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 hayakufanya mabadiliko kwenye lugha ya kufundishia na kujifunzia katika Shule za Sekondari” imeeleza taarifa hiyo.