Kishindo Ngorongoro

0
118

Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Kaika Saning’o Ole Telele amejiandikisha kuondoka kwa hiari ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro.

Akizungumzia uamuzi huo, Ole Telele amesema huo ni uamuzi wake na familia yake na kutoa wito kwa wakazi wengine wa Ngorongoro kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya Taifa na vizazi vijavyo kwa kulinda na kuhifadhi mazingira ya eneo la hifadhi.

Hatua ya Ole Telele imekuja ikiwa ni wiki ya tatu tangu kuanza kwa zoezi la kuwahamisha wakazi wa Ngorongoro wanahama kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi hiyo na kuhamia katika eneo la Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Mbunge huyo wa zamani ametoa wito kwa wakazi wengine kuhama kwa hiari ili kuruhusu shughuli na uhifadhi kuendelea katika eneo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella amemsifu Ole Telele na kusema kuwa uamuzi wa viongozi kama yeye utasaidia kuhamasisha wananchi zaidi kuondoka katika eneo hilo ambalo ni urithi wa dunia.

Mpaka sasa jumla ya kaya 48 zenye wakazi 228 zimeishahama katika eneo la Ngorongoro na kuhamia katika kijiji cha Msomera ili kupisha uhifadhi wa ikolojia wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro