KISHINDO CHA MEMBE AKIREJEA CCM

0
127

Aaliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe ameeleza sababu zilizomfanya arejee CCM ikiwemo kuondoka kwa sababu ambayo ilimfanya atimkie upinzani.

Aidha, amefungunguka jinsi alivyoumia kutokana na uamuzi wa kumwondolea uanachama wa CCM, Chama alichokulia huku akiahidi sasa atafia ndani ya CCM.

Akizungumza katika mkutano wa kumkabidhi kadi yake ya uanachama ambapo pia umehudhuriwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, katika Kijiji cha Rondo, Membe amesema Machi 30 hadi Aprili 1, mwaka huu aliitwa Dodoma, kwenye Mkutano wa Kamati Kuu ya Maadili na Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu, alipewa nafasi na Mwenyekiti wa CCM Taifa kuzungumza na wana CCM.

“Mama yetu, Rais wetu na Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa alinipa nafasi ya kuzungumza na wajumbe wa kamati kuu ya Chama Taifa. Nashukuru kwa kupewa nafasi ile na wajumbe waliliridhia kwa kauli moja nirejee CCM.