Kiongozi wa ACT-Wazalendo kizimbani kwa tuhuma za kusambaza maudhui ya ngono

0
197

Afisa Habari Mwandamizi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dotto Rangimoto amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shitaka la kusambaza maudhui ya ngono kwenye mitandao ya kijamii.

Akisoma hati ya mashitaka Wakili wa Serikali, Ashura Mzava amedai kuwa mshitakiwa huyo kati ya Januari Mosi, 2020 na Februari 26, 2020 maeneo ya Tabata-Kimanga jijini Dar es Salaam alisambaza maudhui ya picha za ngono kwa kutumia simu ya mkononi kwenye mtandao wa Twitter kwa jina la James Michael huku akijua kifanya hivyo ni kosa kisheria.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega amesema dhamana kwa mshtakiwa huyo ipo wazi ambapo ametakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye makazi ya kudumu jijini Dar es Salaam atakayesaini bondi ya shilingi milioni 5.

Mtuhumiwa amekana shitaka hilo na kesi imeahirishwa hadi Novemba 2, 2020 itakapotajwa.