Kiongozi CHADEMA akamatwa baada ya kuachiwa

0
230

Wakili wa kujitegemea Hekima Mwasipu amesema hajui sababu za kukamatwa tena kwa Kiongozi wa Baraza la Wazee CHADEMA, Hashimu Juma.

Wakili Mwasimpu ameeleza hayo baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kumuondolea mashtaka mwenyekiti huyo na kuachiwa na mahakama ambao baada ya muda mfupi Polisi walimkamata tena na kumpeleka kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

“Hatujajua sababu za kukamatwa tena ila amekamatwa baada ya DPP kumuondolea mashtaka ya uchochezi. Tunafatilia suala la dhamana katika Kituo cha Polisi cha Kati,” amesema Mwasipu.

Hashimu Juma alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza Oktoba 7, 2021 akikabiliwa na mashitaka ya uchochezi ikiwemo kosa la kuchapisha taarifa za uongo na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii.