Kindamba : Msimalize kesi kifamilia

0
192


Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amemwagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Henry Mwaibambe, kuhakikisha kesi zote za ukatili wa kijinsia zinafanyiwa kazi na watuhumiwa wanafikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake badala ya kesi hizo kumalizwa kifamilia.

Kindamba ametoa kauli hiyo jijini Tanga wakati wa zoezi la upandaji miti kimkoa, lililofanyika kwenye viwanja vya Usagara.

Amesema kumekua na tabia ya baadhi ya Wazazi na Walezi kukaa na Madawati ya Kijinsia ili wamalize kesi wenyewe badala ya watuhumiwa kukamatwa.

Kindamba amesema hali hiyo inatokana nq kuwa wahalifu wengi ni miongoni mwa Wanafamilia.