KINANA APATA MAPOKEZI MAKUBWA SIMIYU

0
115

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman kinana ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo.

Kinana ametoa wito huo mara baada ya kuwasili wilayani Bariadi mkoani Simiyu akitokea mkoani Mara na kupata mapokezi makubwa.

Amesema Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi wa mfano hasa katika suala la kuwaletea maendeleo Wananchi katika sekta mbambali ikiwa ni pamoja na afya, elimu, miundombinu na katika kumkwamua kiuchumi Mwanamke.

Kinana amewasili
wilayani Bariadi mkoani Simiyu ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua uhai na utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kuzungumza na Wananchi na Wanachama wa chama hicho.