Kina Mbowe kurejeshewa milioni 350

0
160

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua hukumu ya kesi ya uchochezi dhidi ya Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe na wenzake, na kuamuru warejeshewe kiasi cha shilingi milioni 350 walicholipa kama faini.

Uamuzi huo umetolewa hii leo na Jaji wa mahakama hiyo Irvin Mgeta.

Mbowe na wenzake walitiwa hatiani na kuhukumiwa kulipa faini hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyopo mkoani Dar es salaam.