Kina baba tunzeni ujauzito

0
181

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewataka Wanaume kutunza ujauzito wa wenza wao ili watoto wanaozaliwa wawe salama kiafya na wenye akili ya uwezo wa juu na ufanisi (IQ).

“Kila baba anapenda kujisifia mtoto wake ambaye anafaulu vizuri shuleni, lakini kufaulu vizuri kwa mtoto shuleni kunaendana na kutunza ujauzito toka siku unabebwa, kina baba tunzeni ujauzito, suala la afya sio la wataalamu wa afya peke yake ni la kijamii.’ amesisitiza Dkt. Mollel

Ameyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza katika kikao cha 22 mkutano wa 7 wa Bunge la Tanzania, swali lililoulizwa na Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara Agnes Hokororo

Pia Dkt. Mollel amewataka Wanaume kushirikiana na wenza wao katika kila hatua ya ujaizito ili kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.

“Sisi Wanaume tunahitaji kuwa na ownership ya ujauzito wa kina mama toka mama anapobeba mimba tuweze kushirikiana na mama mpaka siku anapojifungua, tukifanya hivyo itatusaidia sana.”ameongeza Naibu Waziri Mollel

Amesema kwa sasa kila kifo kinachotokea cha mama mjamzito wakati anajifungua kinajadiliwa na taarifa inatolewa kwenye sehemu husika lengo likiwa ni kuhakikisha vifo vya aina hiyo vinapungua.