Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na mikakati yake ya kuboresha kilimo cha Karafuu ambacho kimeipatia Zanzibar umaarufu mkubwa.
Kauli iiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Shamata Shaame Khamis
wakati wa mkutano wa Wahariri wa vyombo vya Habari ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuelekea mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika 2023 utakaofanyika Septemba 05,2023 hadi Septemba 08, 2023 nchini Tanzania.
Amesema Zanzibar imeweka nguvu kubwa katika kuendeleza zao la Karafuu kutokana na umuhimu wake Visiwani humo sio tu kwa sekta ya kilimo pekee bali pia kwa sekta ya Utalii.
Waziri Shamata amesema kwa sasa Zanzibar inajivunia kuzalisha Karafuu yenye ubora zaidi ambayo inahitajika katika maeneo mbalimbali duniani.
Kuhusu sekta ya Kilimo Zanzibar, Waziri Shamata amesema inachangia kwa Asilimia 22 katika Pato la Zanzibar.