Kilimo cha JKT kulinda usalama wa chakula

0
109

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax amesema miradi ya kilimo cha kimkakati na uvuvi ya Jeshi la Kujenga Taifa itachangia kwa kiasi kikubwa kulinda usalama wa chakula nchini.

Dkt. Stragomena ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam aliposhiriki katika maadhimisho ya miaka 41 tangu kunzishwa kwa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) na uzinduzi wa kitabu cha miaka 41 ya SUMA JKT.

Dkt. Stergomena amesema JKT imejipanga kukabiliana na uhaba wa mafuta ya kula nchini kwa kuzalisha kwa wingi zao la alizeti pamoja na.michikichi.

Ameitaka JKT kuitumia changamito ya uhaba wa mafuta ya kula nchini kama fursa ya maeneo ya kimkakati kwa kuzalisha mazao ya alizeti na michikichi ili kuisaidia serikali kuziba pengo la mafuta ya kula nchini.