Kila uongozi na style yake

0
180

Rais Samia Suluhu Hassan amewakumbusha Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa kuwa kila uongozi una aina yake, hivyo wasisubiri kutumwa au kushushiwa maelekezo.

Akifunga mafunzo ya Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa yaliyokuwa yakifanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Rais Samia amewataka viongozi hao kutoyumbishwa kwani wanajua wanayofanya kwenye nafasi zao.

Amewataka kuwa na hoja za kutetea maamuzi wanayofanya pale wanapoulizwa juu ya maamuzi waliyochukua, huku akiwatahadharisha kutokuwa wakaidi bali watazame mazingira yanayowazunguka.

“Kwenye uongozi mmefundishwa kuna style tofauti tofauti, mimi sitakushushia wewe kile cha kusema, nataka wewe uwe na ndoto zako nini unataka kufanya kuendana na sheria, kanuni, miongozo ya Serikali, mipango ya Serikali, mikakati ya Serikali…..yote ile iliyopo wewe kwenye eneo lako unaitumiaje ile kutimiza kazi zako kuleta maendeleo pale ulipo…… usisubiri Rais aseme Mkuu wa Mkoa fanya hilo….” Amesema Rais Samia

Aidha, amewakumbusha viongozi hao kuwa na umoja na ushirikiano katika kazi na kuwa na mawasiliano mazuri ili kurahisisha utendaji kazi wa kila siku