Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewataka walimu wakuu kuandikisha wanafunzi bila kigezo cha kutanguliza ada wala michango yoyote
Waziri Ummy amezungumza hayo wakati akitoa taarifa ya wanafunzi walioandikishwa kwa ajili ya elimu ya awali na elimu ya msingi na kuutaja Mkoa wa Manyara kuwa kinara katika zoezi la uandikishaji wanafunzi kwa elimu ya awali ukifuatiwa na mikoa ya Mara, Njombe, na Tanga.
Aidha waziri Ummy amesema kwa mwaka 2022 wanafunzi 1,363,834 wa elimu ya awali wanatarajiwa kuandikishwa na jumla ya wanafunzi 1,581,823 wa shule za msingi wanatarajiwa kuandikishwa kwa mwaka huu wa masomo. Idadi hii ya wanafunzi inajumlisha pia wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Ameongeza kuwa maelezo ya kina ya jinsi wanafunzi walioacha masomo kutokana na ujauzito au utoro yatatolewa na waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi stadi Profesa Joyce Ndalichako
Waziri Ummy amewasisitiza wazazi kuhakikisha watoto wao wanaopaswa kujiunga na shule Kuwa tayari kuwapeleka shule ikiwa pamoja na kuwanunulia sare za shule, viatu, madaftari na vifaa vingine.
Pia amesisitiza kuwa wazazi ambao watoto wao wamechaguliwa shule maalum ila wamejiunga na shule binafsi wanapaswa kutoa taarifa Ili nafasi zao zitolewe kwa wanafunzi wengine waliofanya vizuri