Kijiji cha Makumbusho kuboreshwa ili kukuza utalii wa Kiutamaduni

0
110

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Francis Michael amezindua Mradi wa Uboreshaji wa Kijiji cha Makumbusho ili kukuza utalii wa Kiutamaduni Kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19, jijini Dar es Salaam

Pamoja na kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kazi nzuri inazozifanya katika uhifadhi wa urithi wa asili na utamaduni, amesisitiza fedha za miradi hiyo zitumike kama zilivyopangwa ili kuleta matokeo chanya ya malengo ye fedha hizo.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga alieleza kuwa fedha zilitolewa kwa Kijiji cha Makumbusho zitatekeleza miradi ya Ujenzi wa Nyumba za Asili kwa kufuata Ramani ya Tanzania; Ujenzi wa maumbo ya sura ya nchi, kuakisi Ramani ya Tanzania (Bahari ya Hindi na Ziwa Victoria); Uboreshaji wa Bohari na Maabara za Mikusanyo na Uboreshaji mandhari ya nje ya Kijiji ili kuleta mvuto shawishi kwa wapita njia na kuboresha onesho la kazi za sanaa za mikono.