Kijana aua wanafunzi 19 na walimu wawili

0
105

Watoto 19 na watu wazima wawili wamefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika shule ya msingi Texas Kusini, nchini Marekani.

Mshambuliaji huyo aliyefahamika kama Salvador Ramos alifyatua risasi katika shule ya Robb Elementary ambayo hufundisha wanafunzi kati ya miaka saba hadi 10, kabla ya kuuawa na polisi.

Mtu huyo aliyeripotiwa kuwa na umri wa miaka 18 alikuwa na bunduki ya mkononi, (AR-15 semi-automatic rifle) na imeripotiwa kuwa kabla ya shambulio hilo alimuua bibi yake.

Gavana wa Texas, Greg Abbott amesema mshambuliaji huyo aliacha gari nje kabla ya kuingia shuleni na kufyatua risasi.