Kigahe: Taasisi za umma zitoe huduma kwa weledi

0
122

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ameziagiza taasisi za umma kuendelea kutoa huduma kwa Wafanyabiashara kwa weledi na uadilifu ili kutimiza malengo ya Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

Pia amewaagiza maafisa wa taasisi zinazohudumia Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani Tunduma (OSBP) kupunguza vikwazo vya kibiashara visivyo vya lazima kwa Wafanyabiashara wanaotumia kituo hicho kinachohudumia nchi sita ambazo ni Zambia, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Afrika Kusini na Namibia ili kukuza biashara za mpakani na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hizo.

Kigahe ameyasema hayo wakati wa ziara yake mkoani Songwe ambapo ametembelea ofisi ya mkuu wa mkoa, Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Wakala wa Vipimo (WMA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani Tunduma lengo likiwa ni kujionea utendaji kazi, kusikiliza na kutatua changamoto zilizopo.